ADDIS ABABA Ghasia zaendelea nchini Ethiopia
6 Novemba 2005Matangazo
Ghasia za hapa na pale zilizuka tena jana mjini Adidis Ababa wakati polisi wa mji huo walipokuwa wanajaribu kuzima machafuko yaliyosabaisha vifo vya watu 46 mnamo wiki iliyopita.
Lakini msemaji wa shirika la kutetea haki za binadamu amesema mapambano yaliendelea jana katika mji wa Debre Berhan umbali wa kilometa 150 kutoka Addis Ababa.
Ghasia zilizuka jumanne iliyopita baada ya wafuasi wa vyama vya upinzani kudai kwamba serikali ilifanya udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo mwezi mei,
ambapo chama cha waziri mkuu Meles Zenawi kilishinda.