ADDIS ABABA: Ethiopia yaulaumu Muungano wa Kiislamu
2 Novemba 2006Matangazo
Ethiopia hii leo imesema uwezekano wa kuzuka mapambano ni hali itakayoshindwa kuepukwa,kwa sababu Muungano wa Kiislamu wa Somalia unakataa kukutana kwa mazungumzo ya amani pamoja na serikali ya mpito iliyo dhaifu.Siku moja baada ya majadiliano kushindwa kufanywa nchini Sudan, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Ethiopia, Solomon Abebe amesema,ni jambo lililo dhahiri kuwa wanamgambo wa Kiislamu hawatii maanani mazungumzo ya amani.Ethiopia imekanusha madai kuwa wanajeshi wake wapatao kama 8,000 wapo Somalia,lakini imekiri kuwa imetuma washauri wa kijeshi kusaidia kuilinda serikali ya mpito dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu,ambao baadhi yao wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na Al-Qaeda.