1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Ethiopia yatakiwa kufanya uchunguzi kuhusu vifo vya watu 36 vilivyotokea katika ghasia za uchaguzi.

30 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEym

Mataifa wafadhili ya magharibi jana yameendelea kuibana zaidi serikali ya Ethiopia kufanya uchunguzi kutokana na vifo vya kiasi watu 36 ambao waliuwawa katika ghasia za uchaguzi mwezi huu.

Mataifa hayo yamesema katika taarifa kuwa , pia yanatoa wito wa kuachiliwa huru kwa watu zaidi ya 1,000 ambao walikamatwa baada ya ghasia hizo ambazo zimeikumba nchi hiyo , baada ya uchaguzi wa hapo May 15, ambao upande wa upinzani unadai ulikuwa na udanganyifu.

Wakati huo huo kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na taasisi ya kimataifa ya vyombo vya habari IPI, siku ya Jumanne, serikali ya Ethiopia imewakamata wahariri wa magazeti wanne kwa kile walichodai ni kashifa dhidi ya jeshi la anga la nchi hiyo.

Wahariri hao walikamatwa kutokana na taarifa zilizoandikwa katika magazeti yao kuwa marubani wanane wa jeshi la

Ethiopia ambao walikuwa katika mafunzo nchini Belarus wameomba ukimbizi katika nchi hiyo.

Mahakama moja ya Ethiopia baadaye iliwaacha huru wahariri hao kwa dhamana ya kiasi cha dola 250 kila mmoja.