ADDIS ABABA : Ethiopia yakaribisha milinia mpya
11 Septemba 2007Matangazo
Waethiopia leo usiku wa manane wanakaribisha milinia mpya miaka saba baada ya dunia kwa jumla kufanya hivyo.
Ethiopia hufuata kalenda ya Kikoptik ambayo iko nyuma miaka saba ya ile ya kawaida ya Gregorian.
Waziri Mkuu wa Ethiopia ameilezea sikukuu hiyo ya mapumziko kuwa ni siku ya kufufuka upya kwa Ethiopia lakini watu wengi nchini humo wanasema tafrija za gharama kubwa kuadhimisha siku hiyo zikienda sambamba na hali tete ya kisiasa zinatia dosari shamra shamra hizo.
Onyesho la wanamuziki wa kundi la Black Eyed Peas wa Marekani pekee linagharimu dola 170 kwa kiti sawa na mshahara wa miezi miwili kwa mwananchi wa kawaida wa Ethiopia.