Addis Ababa. Chama tawala nchini Ethiopia kinadai kupata ushindi katika uchaguzi, lakini mjini Addis Ababa upinzani unaibuka kidedea.
17 Mei 2005Chama tawala nchini Ethiopia kimesema kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili kutokana na matokeo ya awali ambayo yamempa wingi mkubwa waziri mkuu Meles Zenawi.
Madai hayo yanakuja licha ya kura nyingi wanazopata wapinzani katika mji mkuu Addis Ababa. Lakini viongozi wa upinzani wanasema kuwa ni mapema mno kwa chama tawala kudai kuwa kimepata ushindi kwa mara ya tatu.
Kutokana na ushindi mkubwa wa upande wa upinzani katika mji mkuu Addis Ababa , waziri mkuu Meles Zenawi ametangaza kupigwa marufuku maandamano ya aina yoyote katika kipindi cha mwezi mmoja. Uchaguzi huo umekuwa ukiangaliwa na wachunguzi wa kimataifa kama ishara ya Bwana Zenawi kukubali mwenendo wa kidemokrasia.