1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Chama tawala kinadai kimeshinda uchaguzi

17 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFCr

Chama tawala nchini Ethiopia kikinukulu matokeo ya mwanzo ya uchaguzi,kinasema kuwa kimeshinda uchaguzi mkuu uliofanywa mwishoni mwa juma.Kwa mujibu wa matokeo hayo,waziri mkuu Meles Zenawi amepata ushindi mkubwa.Madai hayo yametolewa licha ya kuwa upinzani umefanikiwa kupata kura nyingi sana katika mji mkuu,Addis Ababa.Viongozi wa upinzani wanasema,bado ni mapema mno kwa chama tawala kudai kuwa kimeshinda kwa mara ya tatu kwa mfululizo.Upande wa upinzani vile vile umeituhumu serikali kuwa imefanya udanganyifu wa kura na kuwatisha wafuasi wa upinzani.Kwa upande mwingine waziri mkuu Zenawi amepiga marufuku maandamano yote katika mji mkuu kwa muda wa mwezi mmoja.Uchaguzi wa Ethiopia unatazamwa na wasimamizi wa kimataifa kama ni mtihani wa udemokrasia kwa Zenawi.