ADDIS ABABA : AU yahitaji dola milioni 460 kutanuwa kikosi chake Dafur
26 Mei 2005Umoja wa Afrika unahitaji dola milioni 460 ili kuongeza zaidi ya mara tatu kikosi chake cha kulinda amani katika jimbo la Dafur nchini Sudan.
Umoja wa Afrika (AU) wa nchi wanachama 53 unapanga kutowa ombi la kupatiwa fedha hizo katika mkutano wa ahadi za wafadhili nchini Sudan leo hii.
AU umeweka wanajeshi 2,000 kusimamia usitishaji lege lege wa mapigano huko Dafur magharibi mwa Sudan kwa msaada wa fedha wa kimataifa kugharamia shughuli hiyo.
Dhima yake ya kudhibiti vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo tayari vimegharimu maisha ya watu 180,000 kutokana na machafuko ya umwagaji damu,njaa na maradhi inaonekana kuwa mtihani mkubwa kwa uwezo wa shughuli za kulinda amani wa chombo hicho cha Afrika.