ADDIS ABABA : Afrika yaiondolea vikwazo Togo
27 Februari 2005Matangazo
Viongozi wa Kiafrika wameondowa vikwazo dhidi ya Togo baada ya Faure Gnassingbe kujiuzulu Urais wa nchi hiyo.
Vikwazo vya silaha na safari viliwekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS baada ya jeshi la Togo kumuweka Gnassingbe katika wadhifa wa Urais kufuatia kifo cha baba yake aliyekuwa Rais wa Togo Egnassingbe Eyadema mapema mwezi huu.
Abbas Bonfoh ambaye ndie aliyekuwa spika wa bunge atakaimu madaraka ya Urais hadi hapo utakapofanyika uchaguzi wa Rais mwezi wa April.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameukaribisha uamuzi huo wa Ganssingbe ambaye naye amesema atagombania wadhifa huo katika uchaguzi.