1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA Afrika yaadhimisha siku ya watoto

16 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF31

Umoja wa mataifa umesema leo kwamba mabilioni ya fedha zinahitajika kuwasidia watoto walioachwa mayatima baada ya wazazi kufariki dunia kwa sababu ya ukimwi. Idadi ya mayatima inatarajiwa kuongezeka mara mbili kufikia mwaka wa 2010na kiwango cha dola bilioni moja kitahitajika kila mwaka kuwasaidia.

Katika sherehe za kuadhimisha siku ya watoto barani Afrika, Shirika la watoto la umoja mataifa, UNICEF, limesema watoto wengi wanakabiliwa na umaskini unaosababishwa na ugonjwa hatari wa ukimwi. Watoto wengi hawaendi shuleni, hawapati huduma za matibabu, wana matatizo ya kisaikolojia na wanakabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa wa ukimwi.