ACHEH:ujerumani yatoa euro milioni 20 kuwasaidia wahanga watsunami Acheh
18 Desemba 2006Matangazo
Waziri wa maendeleo wa Ujerumani Heidermarie Wieczoerick-Zeul ameahidi usaidizi zaidi kwa wahanga wa Tsunami katika mkoa wa Acheh. Akiwatembelea manusura wa gharika ya Tsunami kwenye eneo la Banda Acheh waziri huyo wa Ujerumani aliahidi hakuna mtu yoyote atakayesahaulika.
Bibi Heidermarie aliweka shada la maua kwenye kaburi ambako watu waliokufa kwenye mkasa huo walizikwa.
Zaidi ya watu laki moja na sabini elfu wanakisiwa waliuwawa kwenye zilzala hiyo iliyotokana na tetemeko la chini ya bahari lililosababisha mawimbi mazito ya Tusnami yaliyokumba eneo hilo miaka miwili iliyopita.
Waziri huyo wa maendeleo wa Ujerumani ameahidi msaada zaidi wa euro milioni 20 za kusaidia ujenzi mpya wa eneo hilo.