ACCRA: Rais Mugabe amealikwa mkutano wa Ureno
2 Novemba 2007Matangazo
Licha ya upinzani wa Uingereza,Umoja wa Ulaya umemualika Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe kuhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Afrika.Mkutano huo utafanywa nchini Ureno katika mwezi wa Desemba.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno, Luis Amado,wakati wa ziara yake katika mji mkuu wa Ghana,Accra alisema,wanachama wote wa Umoja wa Afrika wamepokea mialiko.Hapo awali,Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown alitishia kuwa hatohudhuria mkutano huo wa kilele ikiwa Mugabe ataalikwa.