1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA: Zimbabwe imejitoa katika Jumuiya ya madola COMMONWEALTH,

8 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFuF
kufuatia kurefushwa muda wa kusimamishwa uwanachama wake kwa kuwa inakiuka kanuni za demokrasia. Waziri wa habari wa rais Robert Mugabe alisema kuzuiliwa zaidi uwanachama wa nchi yake, kuliko kubaliwa na mkutano wa viongozi wa Jumuiyo hiyo mjini Abuja nchini Nigeria, ni ushahidi kuwa viongozi wa kibaguzi wa Uingereza na Australia wameuteka nyara mkutano. Suala la Zimbabwe lilizungumzwa muda mrefu na mkutano huo wa siku 4 na limezusha mgawiko mkubwa kupata konekana tangu enzi ya mbaguano wa makabila nchini Afrika Kusini miaka ya 70 na 80, na limezigawa nchi 54 zanachama chini ya msingi ya rangi ya ngozi. Viongozi wanatarajiwa leo kuuzungumzia uamuzi huo wa Zimbabwe.