Abiria 42 wameuawa Zimbabwe kufuatia tangi la gesi kuripuka
16 Novemba 2018Abiria wasiopungua 42 nchini Zimbabwe wamethibishwa kuwa wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mtungi a gesi uliokuwemo ndani ya basi kuripuka .
Habari hizo zimetangazwa na polisi ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika hii leo."Mnamo wakati huu tulio nao tunataambua watu zaidi ya 42 wameuwawa" msemaji wa polisi Chartity Charamba aliliambia shirika la habari la Ufarana AFP jana usiku.
Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali vinasema mtungi huo wa gesi ulikuwa wa abiria mmoja ambae pia amefariki. Kituo cha matangazo cha ZImbabwe-ZBC kimechapisha picha zinazoonyesha jinsi basi hilo lilivyokuwa likiteketea kataika njia kuu inayoelekea mji wa pili kwa ukubwa Bulawayo.
Wiki iliyopita watu 47 waliuwawa pale mabasi mawili yalipogongana katika barabara inayouunganisha mji mkuu Harare na mji wa mashariki wa Rusape.