Abbas, Haniye wakubaliana kuunda kamati ya maridhiano
31 Julai 2023Rais Mahmud Abbas na kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh, walikutana kwa mazungumzo ya nadra ya ana kwa ana katika mji wa pwani wa El-Alamein pamoja na wawakilishi kutoka makundi ya kisiasa ya Kipalestina.
Jaribio hilo la karibuni kabisa la maridhiano linalenga kuziunganisha serikali mbili zinazoendeshwa sambamba za Hamas katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa Israel na ile ya Mamlaka ya Palestina -- inayodhibitiwa na vuguvu la Fatah lake Abbas -- ambalo linatawala katika maeneo yanayoendeshwa na Palestina ya Ukingo wa Magharibi.
Soma zaidi: Pande pinzani nchini Palestina zaandaa mkutano wa pamoja kuhusu Israeli na UAE
Hamas na Fatah wafikia mwafaka wa mshikamano
Abbas na Haniyeh waliungana na wakuu wa makundi mengine, isipokuwa wa kundi lenye nguvu la Islamic Jihad na makundi mengine mawili madogo.
Haniyeh alisema bunge jipya, litakalojumuisha pande zote lazima liundwe kwa msingi wa uchaguzi wa kidemokrasia.
Naye Abbas akasema lazima pande zote zirudi kwenye dola moja, mfumo mmoja, sheria moja na jeshi moja halali.