450,000 wana COVID-19, 7,000 wafa Afrika Kusini
28 Julai 2020Matangazo
Takwimu mpya zinaonyesha kuwa nchi hiyo sasa imethibitisha maambukizi 452,529 ya ugonjwa huo, na jumla ya vifo 7,067, vikiwemo 300 vilivyorikodiwa kwa siku moja.
Afrika Kusini inayo nusu ya maambukizi yote ya virusi vya corona yaliyosajiliwa katika bara zima la Afrika, na inashikilia nafasi ya tano duniani.
Kama ilivyotokea kwingineko duniani, nchi hiyo imeshuhudia wimbi jipya la maambukizi baada ya kujaribu kuzifungua shughuli za kiuchumi.
Makampuni ya biashara yanalalamika, na kiwango cha wasio na ajira kimepanda hadi asilimia 30, kikitarajiwa kuendelea kuongezeka.