Serikali ya Ethiopia imesema kwamba imeudhibiti mji wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Tigray. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed imetangaza leo kupitia televisheni ya taifa kwamba vikosi vya usalama vimechukua udhibiti wa mji wa Adigrat na sasa vinaelekea kwenye mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele.