Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeeleza katia ripoti yake kwamba mwaka 2016 tumeshuhudia ongezeko la, siasa za kuchochea, hofu na chuki. Wanasiasa duniani kote wenye kuzitenganisha jamii, kutumia visigizio, kuzibebesha lawama jamii za wachache, wahamiaji na wakimbizi. Na matokeo ya hayo ni kuporomoka kwa haki za binadamu.