1860 Munich yakabiliwa na hali mbaya ya fedha
1 Juni 2017Hali hiyo ya mkwamo inahatarisha hatima ya klabu hiyo wakati muda maalum uliowekwa na shirikisho la soka la Ujerumani DFB kulipa fedha kwa ajili ya leseni ya kucheza katika daraja la tatu ukikaribia.
1860 ambayo ilishishwa daraja kutoka daraja la pili nchini Ujerumani Jumanne iliyopita na kuelekea katika daraja la tatu , inakabiliwa na kufilisika na kushushwa hadi daraja la nne ama la tano hadi pale itakapoweza kulipa chama cha kandanda cha Ujerumani liseni yake ya daraja la tatu ifikapo Ijumaa mchana.
Makamu wa rais Heinz Schmidt na Hans Sitzberger wanasema katika taarifa kwamba "kabla ya mchezo wa mchujo", Ismaik alikuwa tayari ameeleza nia yake ya kuisaidia timu hiyo kifedha , bila kujali ni ligi gani timu hiyo itacheza, katika idadi kadhaa ya madai ambayo klabu haiwezi kuyatimiza kwa sababu za kisheria na kiutawala. Taarifa kutoka kwa chama cha kandanda zinaunga mkono tathimini yetu, wamesema.