Waziri Mkuu wa Bangladesh leo hii ameelekea Marekani kwa ajili ya kuhudhuria hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa ambapo ataomba msaada wa kimataifa kutokana na janga la wakimbizi la jamii ya Waislamu wa Rohingya na Mgombea wa Ukansela wa chama cha SPD nchini Ujerumani Martin Schulz amezungumza na DW leo na kujieleza msimamo wake kuhusiana na masuala kadha ikiwemo pia mvutano na Uturuki.