Kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio imeanza katika Ukanda wa Gaza. Afisa wa huduma za Afya Moussa Abed wa wizara ya Afya ya Gaza iliyo chini ya Hamas amesema chanjo zimeanza kutolewa Jumamosi ingawa maafisa walisema awali kuwa chanjo hiyo ingeanza rasmi kutolewa Jumapili.