1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Özil aachwa nje ya kikosi

9 Oktoba 2014

Kiungo wa Ujerumani Mesut Özil amewachwa nje ya timu ya Ujerumani itakayoshiriki mechi ya kufuzu katika dimba la Euro 2016 kutokana na jeraha la goti na sasa atakuwa mkekani kwa miezi mitatu.

https://p.dw.com/p/1DSUs
WM 2014 Achtelfinale Deutschland Algerien Özil
Picha: Getty Images

Kwa mujibu wa msemaji wa timu y ataifa ya Ujerumani, Jens Grittner, Özil aliwasili katika kambi ya mazoezi ya Ujerumani akiwa na maumizu katika goti lake la kushoto.

Mchezaji huyo wa Arsenal kisha alisafiri moja kwa moja hadi Munich ili kufanyiwa vipimo na daktari wa kikosi cha Ujerumani, na hakuweza kufanya mazoezi na wenzake.

Wakati huo huo, nahodha wa timu Bastian Schweinsteiger ataendelea kusalia nje ya kikosi cha Ujerumani, kwa sababu ya kifundo cha mguu, wakati kiungo nyota Marco Reus pia akiwa mkekani akiuguza jeraha. Wakati wa mechi mbili zijazo za kufuzu katika kinyang'anyiro cha Euro 2016 dhidi ya Poland na Ireland, nahodha Manuel Neuer atashuka dimbani kama nahodha wa kikosi.

Habari nzuri kwa mashabiki wanaopenda kandanda ya mashambulizi ni kuwa Andre Schürrle na Julian Draxler, ambao walitarajiwa kuukosa mchuano dhidi ya Poland, sasa wana nafasi ya kucheza.

Mwandishi: Bruce Amani/DW
Mhariri: Josephat Charo